Fanya Yafuatayo Kudumisha Mapenzi Kwa Mpenzi Wako
1. Muamini mmeo au mchumba wako.
Hapa nazungumzia uaminifu kati yako na mpenzi wako pia penda kudumisha hilo kwa kua pamoja nae na kumheshimu mwezi wako.
2. Usikatishe tamaa katika maono yake.
Hapa ningependa utambue kuwa kusudi “kuu”la uumbaji wa mwanamke ni “usaidizi” kwa mwanaume..(nitalizungumzia kiundani katika makala maalum).ila tambua kwamba utakapo kuwa msaada tosha na mwaminifu hadi mwenzi wako atakapotimiza malengo yake, ni dhahiri hata yale unayohitaji atakutimizia tena kwa moyo na bila ya kumuomba wala kumsukuma.
3. Usimlazimishe kupenda mambo unayoyapenda.
Ni vyema ukatambua kuwa kama binadamu tunavyotofautiana majina sura pamoja na tabia, haijalishi mahusiano yenu yamefika wapi hamuwezi kwa pamoja mkapenda kila jambo kwa usawa. Wewe hupendi mpira yeye anapenda mpira, yeye havutiwi na tamthiliya wewe unavutiwa sana na tamthiliya. Hapa haina haja ya kumlazimisha aje na awe na machaguo kama yako ,unaweza kumshawishi (kwa vitendo au kusifia na kuhusianisha na maisha yenu) na sio kumlazimisha. ::Wanaume hawapendi kulazimishwa kwani huona kana kwamba wanaburuzwa.
4. Usipange kumbadilisha.
Hili nalo ni changamoto sana kwa wanawake wengi wanaoingia katika mahusiano, SAWA kila mtu huwa na maono ya mwenza anaedhani atamfaa au anaemuhitaji SIKATAI. Ila mpaka umeafiki kuingia nae katika mahusiano ni dhahiri ulijiridhisha kuwa mtaenda au pengine anakufaa, unapoingia kwenye mahusiano kwa lengo la kumbadilisha mtu kwanza kabisa unajiweka katika mazingira ya kuupoteza uhlisia wake ( na huenda mapenzi yakapungua) au ukashindwa kumbadilisha (ukabaki na hali ya kutoridhika) ndio maana huwa nashauri kwamba kabla ya kuanza mahusiano pima nyakati na umuombe Mungu kwa Imani yako ili akupe muongozo na majibu sahihi,kinyume na hapo hizi tunazoita heart-break zitakuwa wimbo wa kila kukicha.
5. Usidhani kwamba hawezi kutambua uwepo na uzuri wa wanawake wengine.
Hapa sasa najua fika kuwa unahisi kama nakukosea heshima hivi (hahahaha) hapana ninamaanisha ninachosema. Zipo tafsiri nyingi za uzuri ila kwa ufupi twende tu na hio ambayo unayo katika mawazo yako kwa sasa. Ni kweli kamwe usidhani kwamba mwenza wako hawezi kukutana, kuona na kutambua uwepo na uzuri wa wanawake wengine lakini kwa kutambua hilo nakupa kama changamoto USILEGEZE KAMBA. Kumekuwa na tabia kwa wanawake kuacha kujiweka sawa, kuonesha mapenzi na mahaba pale mahusiano yanapokolea ama pale mwanaume anapoanza kupunguza baadhi ya vitu, Hii sio sahihi.
Hebu tuutazame mfano huu amabao tunao katika maisha yetu ya kawaida . Tunazo chaneli kadhaa zinazoonesha vipindi vya televisheni lakini hata wewe ipo ile ambayo lazima uitazame mara kwa mara kwakuwa inakuvutia aidha kwa mpangilio wa vipindi au aina ya uwasilishaji LAKINI hii haimaanishi kuwa chaneli ambazo huwa hauzipi kipaumbele kuwa ni mbaya na haizifai kutazamwa. Siku chaneli unayopendelea ikianza kupunguza baadhi ya mambo yaliyokufanya uvutike ni dhahiri utavutika kuanglia na kwingine kuna vipindi vya aina gani na kwakulitambua hilo kiushindani chaneli hizi huweka bidii kila iitwapo leo kuhakikisha inaboresha zaidi na zaidi…Je upo tayari kulegeza kwakuwa amekuchagua wewe????
6. Usilazimishe kuwajibika juu ya mambo yako: Kama vile kwenda saluni, umeme, vocha na mambo mengine hasa kama bado mko katika mchakato wa uchumba, kama atafanya hivyo mwache afanye mwenyewe msimlazimishe eti kwa sababu shosti wako huwa anafanyiwa hivyo na wewe unataka, ladies hicho sio kipimo cha mapenzi.

No comments