Progesterone: Homoni 'inayoweza kupunguza hatari ya kupoteza uja uzito'



Wanawake ambao wamewahi kupotea uja uzito au waliovuja damu katika miezi ya awali ya uja uzito wanaweza kuimarisha nafasi yao kujifungua salama iwapo watapewa homoni ya progesterone, utafiti unaonyesha.
Watafiti nchini Uingereza wamefanya majaribio kwa wanawake 4000 wenye mimba.
Samantha Allen, mwenye umri wa miaka 31, alianza kuvuja damu alipompoteza mwanawe wa kwanza na alifanya hivyo tena alipokuwa mja mzito kwa mara ya pili.
Badaa ya kupewa homoni hiyo kwa wiki naneo, almzaa mwanawe wa kiume Noah.
Progesterone ni homoni muhimu wakati wa uja uzito - inayotumika kuimarisha uzio wa kizazi ambako sehemu ambako kijusi kinajiambatanisha na kusaidia mfumo wa kinga mwilini.
Samantha alipewa tembe za homoni ya progesterone kwa majaribio , ambazo alizitumia mara mbili kwa siku mapaka alipotimiza wiki 16 za uja uzito.
Alisema aliacha kuvuja damu wiki moja tangu aaanze kutumia tembe hizo na aliendelea vizuri na uja uzito wake.
"Natumai hawatoteseka tena, inakuathiri sana," amesema.
Mwanamke mmoja kati ya watano hupoteza mimba, na mara nyingi uvujaji damu unahusishwa na kuongezeka hatari ya mwanamke kupoteza uja uzito.
wakati homni hiyotayari imetumika katika mfumo wa kupachika mimba, IVF, Samantha anasema hakuwa na shida yoyote kushiriki katika utafiti huo.
"Ninafurahi, sikuhisi hatari yoyote kwasbabu yalikuwa hayakuwa majaribio ya kiwango cha awali."
Utafiti huo wa chuo kikuu cha Birmingham uliochapishwa katika jarida la afya la New England, umewahusisha kundi la wanawake 200 waja wazito waliopewa homoni ya progesterone, huku kundi jingine la wanaawake kama hao wakipewa tembe bandia.
Wote walikuwa wanavuja damu katika miezi ya kwanza ya uja uzito.
Misacrriage AfricaHaki miliki ya pichaJEAN CHUNG
Image captionSio wanawake wote wanaovuja damu katika siku za kwanza wanaweza kusaidiwa kwa kutumia homoni hiyo
Licha ya kamba utafiti huo umeonyesha sio wanawake wote wanaovuja damu katika siku za kwanza wanaweza kusaidiwa kwa kutumia homoni hiyo, manufaa hayoni makubwa miongoni mwa wanawake walio na historia ya kupoteza uja uzito. (Watoto watatu au zaidi)
Miongoni mwa wanawake hao, kulikuwa na ongezeko la 15% la wanawake waliojifungua - huku 98 kati ya 137 wakifanikiwa kujifungua ikilinganihswa na 85 kati ya 148 waliopewa tembe hizo bandia.
Arri Coomarasamy, daktari wa afya ya uzazi katika hospitali ya akina mama na watoto Birmingham amesema matibabu hayo huenda yakasaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watoto.
Ameendelea kueleza kwamba matibabu hayo hatahivyo hayatofanya kazi kwa wanawake wanaopteza uja uzito, kwasababu kuna sababu nyingi na ngumu kuhusu kwanini wanawake hupoteza uja uzito.
Ni wanawake walio na tatizo la upungufu wa homoni ndio wanaoweza kufaidika.

No comments