ACHA KUISHI KATIKA NDOTO KUBALI AINA YA MUME ULIYENAYE?

Tatizo lako unaishi katika ndoto, kuna mwanaume wako kichwani ambaye uko naye, wakati unaingia kwenye ndoa huyo mwanaume alikua ni mlevi na malaya. Kila siku ulikua unamfumania, ukadhani kuwa labda ndoa itambadilisha, ukweli ni kwamba ndoa haibadilishi mtu na nadhani sina haja ya kukuambia umeona.
Sasa hivi una maamuzi mawili, kwanza ni kuendelea kudhani kuwa atabadilika, kuendelea na hiyo kazi ya kila sikua kirudi nyumbani kuchukau simu yake, kuikagua na kuwa[pigia simu wanawake zake, kutukanana nao na kuwaambia waachane na mume wako na pili ni kujichagua wewe.
UTAMUZAIDIAPP
Kwanza kukubali kuwa ni mlevi na haachi, pili ni kujiuliza, kama pombe anakunywa yeye, ni starehe zake mimi nafanya nini? Huna kazi, kazi yako ni kupigia wazazi wako, kuwaomba pesa ya kumlisha huyo mwanaume, badilika, omba ndugu zako mtaji, tafguta Biashara na fanya. Unasema kuwa kakukataza kufanya kazi, dada mbona wewe umemkataza pombe na umalaya lakini anakunywa kila siku.
Tafuta kazi, anzisha Biashara, ukipata akikutishia kukuacha muambie kwaheri, tafuta hata chumba chako kimoja ishi na wanao komaa hivyo hivyo. Ukweli nikuwa, unajisumbua, kwa aina ya ulevi wa mume wako, wanawake anaotembea nao wote ni walevi, wanajua kaoa hivyo hata ukiwamabia kuwa amekuoa hawajali, wanachojali ni bia tu watakazonunuliwa.
Kuhusu ndoa yako haiwahusu, utaongea mpaka uchanganyikiwa. Kwa unavyoongea wewe ni wale wanawake ambao mna akili ya maisha lakini hamna akili ya mapenzi. Mume wako anajua kuwa, akikuruhusu ufanye kazi basi utafanikiwa na utamuacha na pombe zake. Ndugu zake washamchoka na mzigo wamekuachia wew2e, hivyo unajisumbua tu kudhani kuwa wataongea naye na atabadilika.
MREJESHO; Mwaka 2017 nilikutafuta ukanishauri kuhusu mume wangu ambaye alikua analewa na wanawake. Uliniambia nitafute kazi, niliumia sana kwani nilikupigia ili unisaidie mume wangu aache pombe lakini wewe ukaniambia nibadilike mimi. Sikukusikiliza mpaka siku mmoja mume wangu aliporudi usiku, alikua amelewa na kunibaka, akanifanyia mapenzi kinyume na maumbile.
Hapo ndipo nilijua kuwa ndoa imekufa, niliamini maneno yako kuwa mimi ndiyo napaswa kubadilika sio yeye. Basi niliamua kutafuta kazi, niliomba pesa nyumbani uili kufungua Biashara alinitishia kuniacha lakini nikamuambia nimechoka kama ananiacha aniache tu njia nyeupe sitakufa. Kanitishia watoto, nilijua kabisa hawezi wachukua, nikamuambia watoto ni wake, hata akitaka kuwachukua awachukue.
Nilifungua Biashara, tukawa tunagombana kila siku. Lakinii sasa hivi nashukur, ndugu zangu wamanisaidia sana, wamenisaidia sana na ni kwasabbu yako, mwanzo walikua wananipa pes aya kula ila walipoona nimepata akili ya Biashara basi wakajitoa na sasa hivi nina duka langu kubwa tu la vyombo. Haniumizi kichwa nalea wanangu yeye bado analewa ila sijali tena, natamani kuondoka kumuacha ila namuonea huruma kwani naona kama atateseka.
KUTOKA KWANGU; Unapoingia kwenye ndoa ni lazima umjue mwanaume wako, ujue yeye ni mtu wa aina gani, ujue tabia zake. Kuna wanawake wanaingia wkenye ndoa wakijua kwua wanaume wao wana tabia flani hivyo kuwaza kuwabadilisha na kuna wanawake ambao wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawajui tabia za wanaume wao lakini nao watataka kuwabadilisha.
Huyo mwanaume ni mtu mzima, anachofanya si kwasababu hajui madhara yake bali ni kwakua kaamua. Acha kumuona kama mtoto, badal aya kupiga kelele kila siku kuwa unataka nabadilike hembu jiulize kwanini wewe hubadiliki, mfano yeye kaamua kupeleka pesa zake kwa wanawake na pombe je wewe unapaleka zako wapi?
Kwanza je unazo zako, kama huna zako kwanini usitafute. Lakin pili kama unazo kwanini usiafanye hivyo vitu unavyomshauri afanye? Dada yangu hakuna mwanaume anayebailika kwa kelele bali anabadilika akiamua yeye na hasa akiona wewe unabadilika.

No comments