MAKOSA KUMI YA KUEPUKA WAKATI WA KUONGEA NA YULE UMPENDAYE!
Leo nakupa dondoo fupi muhimu kuhusu mawasiliano kati yako na umpendaye. Dondoo hizi ni nguzo muhimu katika kuimarisha mawasiliano!
🍎 Tafiti zinaonesha kwamba wanawake wengi wanapenda zaidi mtu mcheshi, muongeaji na msikivu. "Mke wako anaenjoy!" Hiyo ni kauli ambayo mwanaume mcheshi atakutana nayo mara nyingi.
Sasa basi hebu angalia makosa haya machache ambayo yanadunisha ufanisi wa mazungumzo kwa wapendanao!
1. Kusikiliza jambo zito huku ukiendelea na shughuli nyingine kama kupika, kudeki au kuchezea simu.
2. Kumkatisha mwenzio kabla hajamaliza.
3. Kudakia habari katikati na kuiendeleza hadi mwisho.
4. Kukosoa sana. Sio kila kitu lazima ukosoe, kuna stori nyingine hata ukikosoa haileti faida kwenye mazungumzo, ni vizuri ukasikiliza tu na kuendelea kufurahia mazungumzo.
5. Kuwa mbali kimawazo. Unapozungumza na mtu muhimu kwako, onesha usikivu na utulivu wa fikra, lugha ya vitendo, kichwa, macho na mikao yako ioneshe kwamba unamsikikiza kwa makini.
6. Kuuliza maswali ya kukomoa. Unapouliza maswali magumu kwa lengo la kumfanya mwenzio ajione kilaza unaua shauku yake ya kuongea na wewe!
7. Kutojiamini. Mara nyingi husababishwa na aina ya maisha yenu. Kwa mfano kama mke na mume si marafiki, mazungumzo yao hutawaliwa na hofu, vitisho na amri.
8. Kutolea mifano ya mambo mabaya ambayo mpenzi wako alifanya zamani (unavunja kanuni ya msamaha).
9. Kushindwa kuchombeza ili mazungumzo yaendelee. Hili limesababisha watu kuchati zaidi na marafiki kuliko wapenzi wao.
10. Kutozingatia aina ya mazungumzo. Stori inayowaunganisha wote wawili ndio inapaswa kujadiliwa kwa muda mrefu, nyingine zipe muda mfupi.
Mawasiliano ni sanaa, ni lazima ujifunze kwa ufasaha ili kuboresha mahusiano!
Hongera kwa kupata kitu!
No comments